Hadi kufikia sasa,watoto hutumia
dawa zinazotumiwa na watu wazima ambazo hugawanywa kusagwa na kutiwa katika
maji.
Daktari Cherise Scott,mkurugenzi wa
maswala ya magonjwa ya watoto katika muungano wa utengezaji wa dawa za TB
,anasema kuwa dawa hiyo mpya inaweza kuleta afueni kwa watoto milioni moja
ambao huambukizwa kifua kikuu kila mwaka ,pamoja na waangalizi wao.
Kenya ndilo taifa la kwanza kutoa
dawa hiyo mpya kwa raia wake huku mataifa zaidi yakitarajiwa kuendelea na
utoaji wa dawa hizo katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Dawa hiyo ni mchanganyiko wa dawa tatu zinazotumiwa
kutibu Tb,zikiwa zimechanganywa kikamilifu na kuwekwa ladha ili kuwavutia
watoto.
Inaweza kuyayuka kwa urahisi ndani
ya maji,hivyobasi kuifanya kuwa rahisi kutumia kila siku katika kipindi cha
miezi sita.
Hadi kufikia sasa ,waangalizi wa
watoto hulazimika kuzivunja dawa hizo kabla ya kuwapatia watoto hao.Dawa hizo
ambazo ziko uchungu ni vigumu kumeza.
Ugonjwa wa kifua kikuu unaongoza
miongoni mwa magonjwa hatari dunia,na huwaua watu 3000 kila siku.
Dawa hiyo mpya itayasaidia maisha ya watoto zaidi
No comments:
Post a Comment