WAZIRI MKUUkuu Mhe. Kassim Majaliwa ametoa wiki moja kwa
Afisa Elimu Mkoa wa Pwani, Yussuph Kipengele kupeleka walimu wa kufundisha
masomo ya kidato cha tano na sita katika shule za sekondari za Mkongo na Utete
wilayani Rufiji.
Ametoa agizo hilo Jumatatu,
Septemba 26, 2016 wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Jumba la Maendeleo wilayani
Rufiji. baada ya Mbunge wa Rufiji, Muhammed Mchengelwa kumwambia kuwa
wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa walimu wa kidato cha tano
na sita licha ya kuwa na shule.
"Hatuwezi kuwa na shule ambazo
hazina walimu, nasikia hapa anayefundisha ni Mkuu wa shule na mwalimu mmoja tu,
wakati kule Kibaha kuna walimu walmerundikana ,sasa fanya realocation tarehe
4,Oktoba uniletee taarifa walimu wamefika Rufiji.",alisema Waziri
Mkuu.
Akizungumzia suala la upungufu wa
watumishi wa umma kwenye sekta mbalimbali, Waziri Mkuu alisema baada ya kazi ya
uhakiki watumishi hewa itakapokamilika, serikali itaangalia kwenye maeneo yenye
upungufu na hivyo kutangaza ajira.
"Hivi sasa serikali
inakamilisha masuala ya uhakiki wa watumishi, tukimakamilisha na kujua idadi ya
watumishi na maeneo yenye upungufu tutaanza tena kuajiri, tulisitisha kupisha
kwanza kazi hii,alisema Waziri Majaliwa.
Kuhusu migogoro ya wakulima na
wafugaji Waziri, Mkuu alisema watendaji wa halmashauri na vijiji wanapaswa
kutenga maeneo ya wafugaji na wakulima na kutaka mifugo isiongezwe kwenye
maeneo ambayo hayajaruhusiwa.
Alisema wenyeviti wa vijiji
wanapaswa kusimamia utekelezaji wake katika mpango wa matumizi bora ya ardhi na
kwamba atakayeruhusu idadi kubwa ya mifugo kuingia kijijini zaidi ya ile
iliyokubalika atawajibishwa ikiwemo kufukuzwa kazi na hatua nyingine za kisheria.
"Hatuwezi kuendelea kuwa
na watumishi wasio na nidhamu, wale wote watakaoingia mifugo zaidi ya uwezo wa
kijiji wafukuzwe kazi na kuchukuliwa hatua, lakini pia wafugaji ni marufuko
kuingiza mifugo kwenye mazao ya wakulima"alisema Waziri Mkuu.
Kuhusu ujenzi wa barabara ya
lami kwenda makao makuu ya wilaya ya Rufiji, Utete, Waziri Mkuu aliahidi
kuchukua ombi hilo na kusema bajeti ijayo litatengewa fedha kuwa ajili ya
kufanya maandalizi ya upembuzi kuona gharama yake kabla ya kutangaza zabuni ya
ujenzi.
Kuhusu utengenezaji wa
madawati, Waziri Mkuu alisema ifikapo Oktoba 30, mwaka huu kila wilaya nchini
inapaswa iwe imekamilisha utengenezaji wa madawati hayo kwenye shule
nchini.
Aidha, alisema ipo miradi
mingi inayoendeshwa kwa maslahi binafsi ukiwemo mradi wa Bonde la
Rufiji(RUBADA), ambao wamebaini kuna ubabaishaji mkubwa, hivyo wamepeleka timu
ya wataalamu kuhakiki ili wale wabadhirifu wachukuliwe hatua.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI
MKUU,
JUMATATU,
SEPTEMBA 26, 2016
No comments:
Post a Comment