Msanii wa muziki Kala
Jeremiah amewataka wasanii wenzake kufanya nyimbo za kijamii bila kuogopa kama
zitafanya vizuri.
Akiongea
Jumatato hii, Kala amewataka wasanii kuacha kuogopa kufanya muziki wa kijamii
kwa hofu ya kutofanya vizuri.
“Mimi
ningewaambia wasanii wenzangu nyimbo za kijamii ndio nyimbo ambazo zinafanya
vizuri bila taka kuumiza kichwa, nyimbo za kijamii zinalipa sana tofauti na
wasanii wanavyofikiria, mimi nina wimbo wangu ‘Wanandoto’ umefanya vizuri sana,
tena naweza kusimama jukwaani na msanii mwingine lakini mimi nikala shangwe la
kufa mtu.Kwa hiyo mimi nawashauri tu, tuzikumbuke jamii tunazotoka,” alisema
Kala.
Rapper
huyo amesema wimbo ‘Wanandoto’ unampatia deal nyingi kubwa za kijamii tofauti
na baadhi ya wasanii wanavyofikiria.
No comments:
Post a Comment