Wiki kadhaa
zilizopita, D’Banj alitengeneza vichwa vya habari baada ya kudaiwa kuwa
amefunga ndoa kisiri na mpenzi wake, Lineo Didi Kilgrow.
Tangu
hapo, muimbaji huyo amekuwa kimya kuhusiana na suala hilo hadi Jumamosi
iliyopita alipozungumza na Saturday Beats.
Akizungumza
kuhusu ndoa yake, muimbaji huyo alisema maisha yake binafsi hayahusianI na mtu
yeyote na kuwaomba watu kuyaacha maisha ya familia yake faragha.
“Ndoa
yangu ni mambo yangu na si mambo ya mtu mwingine. Kama nimeoa ama sijaoa,
fuatilia mambo yako. Kama ukija kuona pete ya ndoa kwenye kidole changU, sawa,
lakini kama huoni, sawa,” alisema.
“Ukweli
kuhusu hilo ni kwamba ni muhimu sana kujua unachotaka kama brand. Kama brand,
nilitaka kujikita kwenye upande wa biashara na kuweka familia na maisha binafsi
faragha,” aliongeza msanii huyo.
Staa
huyo anatarajia kuachia album yake mpya iitwayo CREAM.

No comments:
Post a Comment