Jeshi la Korea Kusini linasema Korea Kaskazini imerusha
makombora matatu ya masafa marefu baharini saa chache baada ya Rais wa Korea
Kusini Park Geun-hye kukutana na Rais wa Uchina Xi Jinping pambizoni mwa
mkutano mkuu wa nchi 20 zenye zilizostawi zaidi kiuchumi duniani.
Makombora hayo yalirushwa kutoka eneo la Hwangju.
Bi Park ametoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano zaidi na Uchina,
ambayo ni mshirika wa Korea Kaskazini, kuhusu kile alichosema ni uchokozi wa
mara kwa mara wa Pyongyang ambayo imekuwa ikifanya majaribio ya mabomu ya
nyuklia na makombora.
Vyombo vya habari Uchina vimesema Xi amesisitiza pingamizi zake
dhidi ya kujengwa kwa mfumo wa Marekani wa kujikinga dhidi ya makombora nchini
Korea Kusini.
Amesema mpango huo huenda ukazidisha uhasama.

No comments:
Post a Comment