Mwenyekiti wa chemba
ya biashara ya wanawake Jackline Maleko, amesema watanzania wanashabikia
uwekezaji wa mafuta na gesi kwa maneno badala ya kuangalia fursa zilizopo
kuanzisha miradi na kujipatia kipato.
Ameyasema
hayo wakati wa kongamano la nne la watoa huduma wa sekta ya gesi na mafuta.
Amesema
ziko fursa nyingi hususan za kutoa huduma za vya chakula, ujenzi, usafirishaji,
nyumba za kulala wageni na mafunzo ambavyo wawekezaji hutumia mawakala wa
kutoka nje.
“Ninapenda kuwaasa watanzania hii fursa ya kuwa na gesi na oil, tunaishabikia kama vile mpira badala ya kuwa wachezaji tunakuwa washabiki. Hili la kuwa washabiki tutashtukia wenzetu wanafaidi kuliko sisi, mnavyofahamu sasa hivi soko la Afrika mashariki lina allow free movement of goods and services, sasa kama linaruhusu namna hiyo halafu sisi ni watazamaji hatushiriki,”alisema Maleko.

“Tukiangalia
fursa mbalimbali zinazotokana na oil and gesi tutabaki kuandamana
tutabaki kulalamika, wakati ambapo serikali imefanya juhudi za makusudi,
kuwa hata na sera ya public private partnership kuwezesha sekta binafsi kwa
kushirikiana na serikali kuchukua fursa kama hii,”aliongeza.
BY:
EMMY MWAIPOPO

No comments:
Post a Comment