Kimbunga hicho kilifika katika ghuba ya Florida mapema Ijumaa
kikiwa katika kitengo nambari moja, na kusababisha mvua kubwa na upepo.
Gavana Rick Scott ametangaza hali ya tahadhari katika kaunti 51
za jimbo hilo huku wakazi wakijiandaa kwa athari za kimbunga hicho.
Upepo ulioandamana na kimbunga hicho ulifikia kasi ya 80mph
(130km/h) Alhamisi, kwa mujibu wa taasisi ya taifa ya Marekani inayofuatilia
vimbunga.
Maafisa katika mji mkuu wa jimbo hilo Tallahassee, ambao
utakumbwa na kimbunga hicho, wamesema karibu nyumba 70,000 kwa sasa hazina
umeme.
Kimbunga cha mwisho kukumba Florida kilikuwa Wilma Oktoba 2005,
na kilitokea mwaka ambao kimbunga cha Katrina kilitokea.
Kimbunga hicho kilisababisha vifo vya watu watano na uharibifu
wa karibu $23bn (£17bn).
"Hili
linatishia maisha. Hatujashuhudia kimbunga katika miaka mingi," Gavana
Scott amesema.
Ameongeza kwamba maafisa 8,000 wa usalama na uokoaji wamewekwa
tayari kusaidia raia.

No comments:
Post a Comment