
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania,
Profesa Benno Ndulu jana alitolea ufafanuzi hali ya kiuchumi nchini huku
akieleza siri ya kilio kinachovuma cha fedha kupotea mtaani na nyingine
zikidaiwa kufichwa.
Akizungumza na waandishi wa habari
jana jijini Dar es Salaam, Profesa Ndulu alisema kuwa kwakuwa taasisi hiyo
ndiyo inayofahamu fedha zote zilizopo benki na zilizopo mtaani, inafahamu kuwa
hakuna fedha iliyopotea bali fedha zimepotea kwa watu waliokuwa wanazipata kwa
njia ya udanganyifu kwakuwa sasa Serikali imebana mianya hiyo.
“Hakuna fedha iliyopotea, Serikali
imebana shughuli za watu na ‘mission town’ sasa shughuli zote zinafanywa na
Serikali. Hivyo, kwao fedha zimepotea, lakini kwetu hazijapotea,” alisema
Profesa Ndulu.
Hata hivyo, Profesa Ndulu alikiri
kupungua kwa fedha katika mabenki nchini hali iliyopelekea kupunguza kasi ya
utoaji mikopo kwa wananchi. Alisema hali hiyo ilitokana na kuhamishwa fedha za
mashirika ya umma na taasisi kutoka benki za biashara kwenda BoT.
“Fedha hizo zitarudi katika benki
hizo wakati zitakapopelekwa kwenye Halmashauri kwa ajili ya kutekeleza miradi
mbalimbali,” Profesa Ndulu aliahidi.
Katika hatua nyingine, Gavana huyo
wa Benki Kuu alisema kuwa uchumi unatarajiwa kukuwa kwa asilimia 7.2 mwaka huu,
huku akibainisha kuwa moja kati ya sababu zinazopelekea ukuaji huo ni
ongezeko la uzalishaji wa umeme na saraju.
Akizungumzia hali ya deni la taifa,
alisema kuwa deni la taifa la ndani limeongezeka kutoka shilingi trilioni
8.6 Mwezi Desemba mwaka jana hadi shilingi trilioni 10 mwezi Juni mwaka huu.
Profesa Ndulu alibainisha kuwa
wakati deni linalotokana na kukopa ndani likipaa, deni linatokana na ukopaji wa
limepungua baada ya Serikali kupunguza ukopaji nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment