
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
imesema kuwa haihusiki kumtafutia mnufaika wa mkopo ajira badala yake
inahusika kumpatia mwanafunzi mkopo na akishamaliza muda wa masomo atatakiwa
kurejesha mkopo wake.
Hayo yamesemwa jana Jijini
Dar es salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Cosmas Mwaisobwa wakati akijibu maswali ya
wananchi kupitia kipengele cha Kikaango cha EATV.
“Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
inatoa mikopo suala la kutafuta ajira halituhusu hivyo mnufaika yoyote asiwe na
kigezo kwamba hajapata kazi , hiyo siyo kazi yetu, kazi yetu ni kuwawezesha
kupata elimu basi”Alisema Mwaisobwa.
Aidha Mwaisobwa alisema wanufaika
wote ambao walipata mikopo wanatakiwa kukatwa asilimia 8% ya pato la mwezi, na
kama mtu anafanya kazi binafsi na hakatwi popote atatakiwa kutoa kiwango cha
120,000/= na kwa ambao wamenufaika na hawataki kuanza kulipa mkopo watapigwa
penati ya 10% ya mkopo kwa mwaka.
Pamoja na hayo Bodi ya Mikopo ya
Elimu ya Juu imewataka walioomba mikopo kuvuta subira kwani Bodi inasubiri
majina kutoka Tume ya Vyuo Vikuu ili Bodi ya Mikopo iweze kufahamu vyuo
walivyopangiwa na kiwango cha ada ili haki iweze kutendeka kwa waombaji.
No comments:
Post a Comment