Jopo linalotoa tuzo za Oscar pia limeidhinisha kutuzwa kwa
mhariri Anne Coates, mwelekezi Lynn Stalmaster na mwandalizi wa filamu za
makala Frederick Wiseman.
Rais wa jopo hilo Cheryl Boone Isaacs amewataja wanne hao kama
"waasisi halisi na stadi katika kazi waliyoifanya".
Chan, 62, alikuwa mwigizaji nyota katika filamu nyingi za
kung-fu zilizoandaliwa katika nchi yake ya kuzaliwa, Hong Kong.
Alivuma kimataifa kwa filamu kama vile Rumble in the Bronx, Rush
Hour na filamu ya vibonzo ya Kung Fu Panda.

No comments:
Post a Comment