Mkazi wa
Mandewa, Manispaa ya Singida, Said Mamba (24), amelazwa katika hospitali ya
mkoa mjini Singida baada ya kung’atwa theluthi tatu ya ulimi wake na mwanamke
waliyekuwa wakinyonyana ndimi.
Tukio hilo la aina yake lilitokea Septemba 12, saa 3:30 usiku wa sikukuu ya Idd el Hajj.
Mamba, ambaye
hawezi kuzungumza ametoa maelezo ya tukio hilo kwa njia ya maandishi.
Alisema siku ya tukio alikutana na mwanamke huyo kwenye grosari iliyopo eneo la Mandewa na baadaye mwanamama huyo alimwomba amsindikize nyumbani kwake.
Alisema siku ya tukio alikutana na mwanamke huyo kwenye grosari iliyopo eneo la Mandewa na baadaye mwanamama huyo alimwomba amsindikize nyumbani kwake.
“Nilikubali
kumsindikiza, tukiwa njiani aliniomba tufanye mapenzi. Nilipokataa
alinilazimisha na baada ya kuona sitaki aliomba tuagane kwa kunyonyana ndimi,
nilikubali ombi hilo,” alisema.
Mamba alisema
wakati wakiendelea, mwanamke huyo alianza kumvua mkanda wa suruali lakini
alimzuia ndipo alipomng’ata ulimi na kuondoka na kipande.
Mzazi wa Mamba,
Fatuma Alli alisema alipata taarifa ya tukio hilo baada ya siku tatu na kwamba,
siku hiyo hiyo mume wa mwanamke aliyetenda kitendo hicho alikwenda kwake akieleza
kijana huyo alijaribu kumbaka mkewe.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Singida, Peter Kakamba, alisema hana taarifa za tukio
hilo.
Daktari wa meno wa hospitali hiyo, Dk Hamisi Kakandilo alisema ulimi wa kijana huyo hauwezi kutibika isipokuwa kuusafisha ili asipate maambukizi.
“Hata kama kipande kilichotolewa kingepatikana kisingeweza kushonwa,” alisema.

No comments:
Post a Comment