Kokeini yenye thamani
ya bei ya mtaani kiasi cha Euro 50 m imegundulika katika kiwanda cha a
Coca-Cola kilichopo kusini mwa Ufaransa.
Dawa
hiyo iliyokuwa imefichwa kwenye mifuko ya kuuzia juisi ya machungwa , ilifika
kwenye shehena kutoka Amerika Kusini
Uchunguzi
unaendelea katika kijiji cha Signes, kilichopo kusini mwa Ufaransa.
|#Marseille|
Var: 370 kilos de cocaïne saisis dans un container de Coca-Cola: La marchandise
illicite valait … https://t.co/hQI4sWLx3S
— DirectMarseille
(@DirectMarseille) August 31, 2016
Kukamatwa
kwa kilo 370kg za kokeini kunafanya kiwango hicho kuwa kikubwa zaidi kuwahi
kupatikana kwenye ardhi ya Ufaransa.
Mwendesha
mashtaka mjini Toulon, Xavier Tarabeux, amesema kuwa bei ya mtaani ya dawa hiyo
ya kulevya ni “Euro milioni 50″ na kwamba ni tukio baya sana la kushangaza”.
Wafanyakazi
wa kiwanda cha Coca-Cola wamekataa kuhusishwa kama wachunguzi wa chanzo cha
mihadarati hiyo .
”
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa wafanyakazi wa kiwanda hizo hawahusiki kwa
vyovyote vile ,” alieleza rais wa kikanda wa Coca-Cola Jean-Denis Malgras,
Mwezi
Aprili 2015, maafisa wa forodha wa Ufaransa walisaidia katika kuwamakata
wanaume wawili waliokamatwa walipokuwa wakijaribu kuendesha manuari iliyokuwa
imesheheni kilo 250 za kokeini hadi Uingereza.

No comments:
Post a Comment