Aliandika kwenye Twitter:
"Sasa sijiwezi tena, haka kiakili, na naondoka kwa staha na nashukuru
mashabiki wangu."
Hata hivyo, hajafafanua iwapo
ataacha sekta ya uimbaji kabisa, au ataacha tu uimbaji wa muziki wa kufoka.
Mwanamuziki huyo wa umri wa miaka
33 hata hivyo amesema hataki "kuonewa huruma".
Lil Wayne amekuwa akigonga vichwa
vya habari hivi karibuni kwa visa mbalimbali.
Amekuwa an mzozo wa muda mrefu na
Cash Money Records kuhusu kucheleweshwa kwa albamu yake ya 11, ambayo imepewa
jina Tha Carter V.
Alishutumu
kampuni hiyo siku mbili zilizopita akitumbuiza na Drake mjini Miami.
Polisi Miami walifika nyumbani kwake kisiwa cha La Gorce baada
ya mtu kupiga simu 911 akisema kulikuwa na ufyatuaji risasi. Habari hizo
hazikuwa za kweli.
No comments:
Post a Comment