Serikali imesema
imejipanga kuishirikisha mifuko ya jamii kikamilifu katika kuhakikisha mchango
wake unatumika kikamilifu kuleta maendeleo na uchumi wa viwanda.
Kauli
hiyo imetolewa mkoani Dodoma na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu, sera,
bunge, kazi, vijana,ajira na wenye ulemavu, Jenista Muhagama, wakati wa mkutano
ulioshirikisha watengaji wa wizara nne.
“Juzi
NSSF wamekabidhi cheki ya bilioni kama mbili pointi moja tayari kwa utekelezaji
wa ujenzi wa viwanda katika nchi yetu ya Tanzania, kiwanda cha kuua vijidudu na
hasa viluwiluwi vinavyozalisha Malaria pale kibaha,” alisema.
“BC
wameshapokea pesa kupitia benki ya Azania, sasa kazi kwako mzee wa viwanda,
simama imara pale, kiwanda kile kifanye kazi vizuri,fedha yetu ya mifuko ya
wanachama iweze kurejeshwa kwa wakati na kwa faida,” alisema Muhagama.
Pia
Muhagama aliongezea kuwa lengo la kuanisha mchango wa mifuko ya hifadhi ya
jamii ni kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa viwanda kufikia mwaka 2025.
BY:
EMMY MWAIPOPO
No comments:
Post a Comment