Zuckerberg aliyewasili siku ya Jumatano kutoka nchini Nigeria
alifanya kikao na waziri wa habari nchini Kenya Joseph Mucheru,ambapo
walizungumza kuhusu mtandao na mipango ya serikali kuhakikisha kila kijiji
kimeunganishwa na mtandao.
Baadaye Zuckerbag aliekea katika hoteli ya Mama Oliech katika
chakula cha mchana ambapo kwa mara ya kwanza alikula Ugali na Samaki.
''Swala muhimu ninapozuru taifa lolote jipya ni kujaribu kula
chakula chao.Nilipenda sana ugali na samaki mzima wa tilapia'',alisema
Zuckerberg.

No comments:
Post a Comment