Mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa
miezi mitano ana chembe chembe za DNA kutoka kwa mamake, babake pamoja na jeni
za mfadhili.
Madaktari wa Marekani walichukua
hatua hiyo kuhakikisha kuwa mtoto huyo wa kiume atakuwa huru kutokana na hali
ya jeni ambayo mamake kutoka Jordan anabeba katika jeni zake.
Wataalam wanasema kuwa hatua hiyo
ni mwamko mpya wa kimatibabu na inaweza kusaidia familia nyingine zilizo na
hali za jeni zisizokuwa za kawaida.
Lakini wameonya kuwa uchunguzi wa
mara kwa mara wa mbinu hiyo mpya ya kiteknolojia inayoitwa ufadhili wa
Mitochondrial unahitajika.
Mitochondria ni vyumba vidogo
vidogo ndani ya kila seli ambavyo hubadili chakula kuwa nguvu inayotumika
mwilini.
Baadhi ya wanawake hubeba jeni
zilizo na kasoro na wanaweza kupitisha jeni hizo hadi kwa watoto wao.
Wanasayansi waliohusika katika
shughuli hiyo walisafiri hadi Mexico kwa sababu huko hakuna sheria za kuzuia
shughuli kama hiyo ya kimatibabu.
Walichukua sehemu muhimu za chembe
za kinasaba (DNA) kutoka kwa yai la mama, na DNA ya mitochondria kutoka kwa yai
la mfadhili na kuunda yai lenye afya ambalo lilitungshwa mbegu kutoka kwa baba.
Matokeo yake ni kuzaliwa kwa mtoto
mwenye 0.1% ya DNA kutoka kwa mfadhili na jeni nyingine zote, zinazoamua sifa
kaa vile rangi ya nywele na macho kutoka kwa mama na baba.
Dkt John Zhang, mkurugenzi wa kimatibabu katika hospitali ya New Hope
Fertility Centre jijini New York City, anasema yeye na wenzake walitumia njia
hiyo kupata viinitete vitano, lakini wakastawisha kimoja tu.
No comments:
Post a Comment