Magari aina ya Audi,BMW na Mercedes Benz yalio na sensa yatakuwa yakigawana habari kuhusu maeneo ya kuegesha magari na marekebisho ya barabara kupitia huduma ya ramani ya kidijitali.
Pia magari hayo yatakusanya data
kuhusu mazingira ya msongamano wa magari ,hatari na ishara za barabarani.
Huduma hiyo inayotolewa na kampuni
ya Mapping inayomilikiwa na kundi moja la watengezaji magari itaanza mwaka
ujao.
Huduma hiyo itarekodi kasi ya
magari,eneo la gari,mwelekeo, breki za ghafla na taa za ukungu.
Picha za video za hatari iliopo barabarani pia
zitaonekana na kamera inayoangalia mbele.
Wamiliki wa magari hayo hawatafanya
lolote kupokea ama kusambaza data, lakini watalazimika kuingia katika programu
hiyo kwa kutumia simu aina smartphone
No comments:
Post a Comment