1,000 katika kipindi cha BBC,
umegundua kuwa 52% waliuguwa, lakini 27% waliwaarifu waajiri wao kwamba ni
mamumivu yanayotoka na hedhi.
52% pekee, karibu thuluthi yao
waliomba kwenda nyumbani japo kwa siku kutokana na maumivu ya hedhi.
Na daktari mmoja amependekeza
waajiri sasa waanze kutoa ''siku ya mapumziko ya hedhi'' kwa wanawake.
Wanawake 9 kati ya 10 wameeleza
kuwahi kuugua maumivu ya hedhi kwa wakati mmoja.
Daktari wa magonjwa ya wanawake kutoka London Gedis
Grudzinskas, anasema wanawake wanapaswa kuwa na uwazi zaidi kuhusu tatizo hili
na waajiri wawe ni wenye kuwaelewa.
Ameongeza: "kupata hedhi ni
jambo la kawaida, lakini baadhi ya wanawake huteseka sana kimya.
"sidhani wanawake wanapswa
kuona haya kuhusu tatizo hili na kampuni zinapaswa kuwaelewa kwa naman
wanavyotaabika kwa uchungu wanao uhisi."
Dr Grudzinskas anasema njia moja ni
kutoa likizo au amapumziko ya hedhi kwa wafanyakazi wote wanawake kama ilivyo
sasa kwa nchi kama Japan.
"Mapumziko hayo yatafanya kila
mtu afanye kazi vizuri ambalo ni jambo lenye manufaa," amesema.
"Hakuna uelewa wa kutosha
kuhusu maumivu au uchungu huo na kuwa huenda maumivu hayo wakatimwingine
yanadhihirisha ugonjwa mkubwa zaidi ''.
"Watu husahau kuwa wanawake ni
nusu ya nguvu kazi, iwapo watahisi wanaungwa mkono , itakuwa ni furaha na
ufanisi wa kila mtu."
No comments:
Post a Comment