HALI ya afya ya Spika mstaafu,
Samuel Sitta si nzuri,baada ya Serikali kumpeleka nchini Ujerumani kwa matibabu
zaidi.
Habari za uhakika zinasema
Sitta alipelekwa Ujerumani juzi kwa matibabu baada ya afya yake kubadilika
ghafla.
“Nilimtembelea siku moja kabla ya
kupelekwa nje ya nchi, kwa kweli hali ya afya yake ilikuwa imedhoofu, namwombea
Mungu amsaidia apone haraka ili arudi kuendelea na majukumu yake.
“Nimesikitishwa mno na taarifa za
kuzushiwa kifo mzee wangu huyu, Mungu ni mwema najua bado anampigania uhai
wake…hii tabia ya mitandao ya kijamii kumzushia mtu kifo sijui inafaidika nini.
“Mpaka anaondoka nchini kwenda
matibabu natambua amekuwa asikumbuliwa mno na tatizo la miguu, sasa mimi si
daktari wake siwezi kuongeza zaidi,”kilisema chanzo chetu.
Septemba 19, mwaka huu, Rais Dk.
John Magufuli alimtembelea Sitta hospitalini alikolazwa kwa muda sasa kumjulia
hali, kisha kumwombea dua Mungu amsaidie.
Siku iliyofuata Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa naye alimtembelea hospitalini kumjulia hali.
Sitta ameshika nyadhifa
mbalimbali, zikiwamo za Spika wa Bunge kuanzia mwaka 2005 hadi 2010, uwaziri na
ubunge kwa kipindi kirefu.
No comments:
Post a Comment