
Mahakama ya Hakimu Mkazi ya
Bukombe mkoani Geita imemhukumu Mwalimu wa Shule ya Msingi Umoja, Daniel
Nyingati kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Sh milioni 1.6 baada ya
kupatikana na makosa ya kuomba na kupokea rushwa.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi na
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bukombe, Gabriel Kurwijila.
Alisema mshitakiwa Nyingati
amekutwa na hatia ya kuomba rushwa ya Sh 130,000 kutoka kwa
Marco Elias aweze kumdahili mtoto wake aliyekuwa amehitimu masomo
ya shule ya msingi kinyume na sheria.
Hakimu Kurwijila
alisema ushahidi ulitolewa mahakamani pande zote mbele ya
waendesha mashitaka kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kudhibiti Rushwa Tanzania
(Takukuru), Kelvin Murusuri na Husna Kiboko umejitosheleza na kumtia
hatiani mwalimu Nyingati.
Alisema mahakama inamhukumu mwalimu
Nyingati kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Sh milioni 1.6 kwa kuwa
alitenda kosa la kuomba na kupokea rushwa.
No comments:
Post a Comment