Kadhalika wamejibizana kuhusu Vita
vya Iraq na juhudi za kukabiliana na kundi linalojiita Islamic State.
Msimamizi wa mdahalo huo Lester
Holt amemwuliza mgombea wa chama cha Republican Donald Trump mbona kufikia sasa
bado hajaweza wazi taarifa zake za ulipaji kodi.
Mgombea wa chama cha Democratic
Hillary Clinton amemshutumu mpinzani huyo wake akisema amekuwa akikwepa kulipa
kodi na kudokeza kwamba hilo lina maana kwamba hakuwezi kuwa na wanajeshi, pesa
za kulipa wanajeshi waliostaafu pamoja na kufadhili elimu na huduma ya afya.
Lakini tajiri huyo kutoka New York
amejibu kwa kusema kwamba atatoa hadharani taarifa hizo iwapo Bi Clinton naye
atakubali kutoa barua pepe 33,000 ambazo zilifutwa kutoka kwa sava yake wakati
wa uchunguzi kuhusu tuhuma kwamba alitumia barua pepe ya kibinafsi kwa kazi rasmi
alipokuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani.
Bi Clinton amekubali lawama kuhusu
kosa hilo na kusema hakuwezi kuwa na "kisingizio".
Kadhalika, Bw Trump amemlaumu
mpinzani huyo wake kuhusu kupotea kwa ajira akisema nafasi za kazi
"zinaikimbia nchi" na akalaumu mikataba duni ya kibiashara.
Amesema Bi Clinton amekuwa mtu wa
"maneno mengi, bila vitendo".
Bi Clinton ameahidi kuongeza
uwekezaji na kuahidi kuunda nafasi takriban 10 milioni za kazi.
Mdahalo huo ulioandaliwa jijini New
York huenda ukawa mdahala uliotazamwa na watu wengi zaidi katika historia
ambapo watu 100 milioni inakadiriwa walitazama mdahalo huo.
Kura za maoni zinaonyesha wawili
hao wanakaribiana sana katika uungwaji mkono.
Mambo mengine makuu yaliyoibuka kwenye madahalo:
§
"Umekuwa ukikabiliana na ISIS maisha yako yote,'' Bw Trump
amemkejeli Bi Clinton
§
Amesema Bi Clinton hana uwezo wa kikudhibiti ukali wa
kumuwezesha kuwa rais.
§
Wamarekani Weusi wanaishi "katika jehanamu" nchini
Marekani, Trump amesema, kwa sababu maisha yao yamekuwa hatari sana.
§
Akijibu kupigwa risasi kwa watu weusi, bw Trump amesema suluhu
ni kurejesha utawala wa sheria.
§
Bi Clinton amesema akichaguliwa kuwa rais atatekeleza mageuzi
katika mfumo wa sheria kwa sababu "suala la asili limekuwa likiamua
mengi".
No comments:
Post a Comment