Na Dotto Mwaibale
KUNDI la uhalifu la watoto wenye
umri kuanzia miaka 18 hadi 25 maarufu kama panya road linatishia usalama wa
wananchi na mali zao maeneo ya Moshi Baa na vitongoji vingine katika Manispaa
ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Kufuatia kukithiri kwa vitendo
hivyo katika kipindi kisichopungua wiki mbili tayari watoto watatu walikuwa
wakidaiwa kuhusika na kundi hilo wameuawa na wananchi wenye hasira kali.
Akizungumza na mwandishi wa habari
hii Dar es Salaa jana mkazi wa eneo la Moshi Baa Relini
aliyejitambulisha kwa jina la Mwarami Abubakar alisema hali sio shwari katika
eneo kufuatia matukio ya kila siku ya kuvamiwa wananchi kujeruhiwa na kuporwa
mali zao na kundi hilo.
"Tayari vijana wawili wiki
iliyopita wamechomwa moto na wananchi wenye hasira huku mwingine akipigwa juzi
hadi kutolewa utumbo na kufariki papo hapo," alisema Abubakar.
Mkazi mwingine wa eneo la Kwa
Mkolemba Khamisi Fadhil alisema kundi hilo limekuwa likifanya vitendo hivyo
mchana kweupe na wanatembea kuanzia vijana nane hadi 10 wakiwa na silaha za
jadi kama nondo, visu na mapanga na mtu yeyote wanayekutana naye ni lazima
wampige na kumpora.
Wenye maduka wanalazimika kufunga
kuanzia saa moja jioni kuhofia kundi hilo ambalo huvunja milango ya nyumba na
kufanya uporaji" alisema Fadhil.
Fadhil alisema maeneo ambayo vijana
hao wameshamiri ni Moshi Baa Relini, Kwa Mkolemba, Diwani na Bomba mbili.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi
wa Ilala, Kamishna Msaidizi (ACP), Salum Hamdan alisema polisi imejipanga
vilivyokukabiliana na vitendo hivyo katika mkoa wake.
"Kwanza napenda kukuambia
kwamba hakuna kundi linalojiita panya road wote tunawahesabu ni wahalifu kama
walivyo wahalifu wengine na hivi ninavyongea na wewe tupo katika siku ya sita
ya operesheni ya kukakamta watu wanaojihusisha na uhalifu wa ujambazi wakiwemo
wanaouza pombe haramu ya gongo," alisema Kamanda Hamdan.
Aliongeza kuwa katika mkoa wake
hivi karibuni utakuwa shwari baada ya askari wake kusambaratisha watu hao
wanaofanya vitendo hivyo.
Imeandaliwa na mtandao wa www.
habari za jamii.com-simu namba
0712-727062
No comments:
Post a Comment