Kiongozi wa wanafunzi katika chuo cha Witwatersrand
nchini Afrika Kusini ameonya kuwa wanafunzi watavuruga shughuli zote nchini
humo ikiwa matakwa yao ya kupewa elimu ya bure hayatatimizwa juma hili.
Onyo la kiongozi wa baraza
linalowakilosha wanafunzi Kefentse Mkhari, linatolewa baaada ya maandamano
yenye ghasia kuzuka kwenye mji mkuu Johannesbug wiki iliyopita, baada ya
serikali kutoa pendekezo kuwa itaongeza karo kwa hadi asilimia nane mwaka ujao.
"Kwa sasa tunataka elimu ya
bure na kama serikali haitajitolea kutupa elimu ya bure , basi tutaifanya nchi
hii isitawalike,"alisema Mkhari.
No comments:
Post a Comment