Mgogoro ndani ya Chama cha
Wananchi (CUF) bado unafukuta ambapo jana Prof. Ibrahim Lipumba, aligomea
mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho ulioitishwa leo visiwani
Zanzibar
Alisema, taarifa zilizotolewa kwa
vyombo vya habari kuhusu kufanyika kwa mkutano huo hazitambui kwa kuwa, mamlaka
zinazohusika kuitisha kikao hicho hazijakidhi matakwa.
Akizungumza na waandishi wa habari
katika Ofisi Kuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es Salaam kupitia taarifa
iliyoandaliwa na Magdalena Sakaya, Naibu Katibu Mkuu Bara aliyesimamishwa na
chama hicho alisema, matakwa ya katiba hayakuzingatiwa.
“Wajibu wa Kamati ya Utendaji ya
Taifa utakuwa kuandaa.. agenda za Baraza Kuu la Uongozi la Taifa na kutayarisha
na kuhifadhi mihtusari ya vikao vyote vya Mkutano Mkuu wa Taifa, Baraza Kuu la
Uongozi la Taifa na vya kamati ya utendaji ya taifa yenyewe na kuwasilisha
taarifa ya yatokanayo kutokana na utekelezaji wa maamuzi ya kikao kilichohusika
kilichopita,” Prof. Lipumba amenukuu katiba ya chama hicho ibara ya 85(5).
Prof. Lipumba alisema, Maalim Seif
Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa chama hicho yupo nje ya nchi na kwamba, kutokana
na Katiba ya CUF,Naibu Katibu Mkuu atakayemfuata Katibu Mkuu kwa madaraka ni
yule aliyetoka upande tofauti wa Jamhuri ya Muungano na upande anaotoka Katibu
Mkuu
Kwa upande wake Magdalena
Sakaya, Naibu Katibu Mkuu Bara aliyesimamishwa alisema;
"Mimi sijaitisha wala sina
taarifa ya kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika Zanzibar, kwa
taarifa nilizonazo hakuna wajumbe wa kamati ya utendaji kutoka Bara waliokua
Zanzibar wakati wa kikao hicho. Nachukua nafasi kuwajulisha wajumbe wote wa
baraza kuu kuwa hakuna kikao chochote cha baraza kuu kilichoandaliwa na kamati
ya utendaji ya Taifa ambayo kikatiba mimi ndiye mwenyekiti wake wakati katibu mkuu
hayupo.
“Mimi ndiye mwenye mamlaka ya
Katibu Mkuu kwa sababu Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara kikatiba ndiye
msimamizi namba moja wa Katibu Mkuu” .
Alisema, Katiba ya CUF ya mwaka
1992 Toleo la 2014 kifungu cha 95 (3) kinaeleza “Naibu Katibu Mkuu
atakayemfuata Katibu Mkuu kwa madaraka ni yule aliyetoka upande tofauti wa
Jamhuri ya Muungano na upande anaotoka Katibu Mkuu,” na kwamba, Katibu
Mkuu anatoka Zanzibar na yeye anatoka Bara.
Hata hivyo Prof. alisisitiza kuwa,
Sakaya hana taarifa ya kikao hicho cha kamati tendaji kilichofanyika Zanzibar.
Pamoja na kuwepo kwa sintofahamu
kutokana na uamuzi wa Jaji Mutungi kumtambua Prof. Lipumba kuwa mwenyekiti
halali wa chama hicho, (Lipumba) amepongeza kurejeshwa kwake.
Prof. Lipumba, mwenyekiti wa chama
hicho aliyesimamishwa na CUF mwezi uliopita, alirejea kwenye nafasi hiyo kwa
kauli ya Jaji Mutungu, Msajili wa Vyama vya Siasa nchini.
Prof. Lipumba alieleza kushangazwa
na hatua ya Jaji Mutungi kukosolewa na baadhi ya wanasheria na majaji mashuhuri
kuwa, hakuna sheria inayompa furasa jaji huyo kuchukua hatua aliyoichukua.
No comments:
Post a Comment