Watafiti wa
Kizungu wanakesha kufanya tafiti chungu mzima na zingine majibu yake zinaweza
kukuacha mdomo wazi.
Kwa mfano huu –
jamaa eti wamebaini kuwa kushiriki tendo la ndoa mara nyingi kunaongeza imani
ya kiroho na hata imani kwa Mungu! Makubwa..
Kwa mujibu wa
utafiti, tendo la ndoa hutoa homoni ya upendo iitwayo oxytocin ambayo haiishi
tu kutengeneza ukaribu wa kijamii bali pia imani ya Mungu – hususan kwa
wanaume.
Watafiti katika
chuo kikuu cha Duke cha North Carolina, wanasema kuwa tendo hilo huhamasisha
imani – ama kuongeza imani katika Mungu na dini.
Utafiti huo
umeliochapishwa mwishoni mwa wiki unaangalia homoni ya oxytocin ambayo huamshwa
zaidi wakati wa kufanya mapenzi, wakati wa kuzaa na wakati wa kunyonyesha.
No comments:
Post a Comment