
VIJANA watano
wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumdhalilisha Rais Dk. John Magufuli na
Jeshi la Polisi kutokana na mauaji ya askari polisi wanne waliouawa na
majambazi katika eneo la Mbande na Vikindu, Dar es Salaam hivi karibuni.
Washtakiwa hao
walifikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele
ya mahakimu watano tofauti na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Salum
Mohammed.
Walisomewa
mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Emmilius Mchauru, Huruma Shahidi,
Margareth Bankika, Dk. Yohana Yongolo na Respicius Mwijage.
Akisomewa
mashtaka, mshtakiwa Dennis Mtegwa anadaiwa Agosti 24, mwaka huu eneo la Ubungo
External kupitia mtandao wa WhatsApp, aliweka maoni katika group linaloitwa Dsm
11 4u Movement, akisema ‘JPM sijui anawaza nini kichwani… hata samahani
hajui au nilikosea hajui’, ‘nchi imefika hapa kwa sababu ya mtu mmoja aliyeamua
kujilipua ufahamu wake’, ‘sijaona tatizo kwa hilo, ila kwa huyu bwana misimamo
ambaye amesema msinijaribu na ilhali kajaribiwa na ubwabwa wa jubilee kusema
yote’.
‘Siasa si chuki wala upinzani si uadui, ajifunze kushindana kwa hoja sio
mitutu ya bunduki na mazoezi yasiyo na kichwa wala miguu ya polisi’.
Mshtakiwa
Suleiman Saidi anadaiwa Agosti 25, mwaka huu maeneo ya Kigogo, kwa kutumia
mtandao wa Facebook, aliandika ‘Safi sana aisee, mi naona wangekufa kama 20
hivi halafu Simon Sirro tumuulize mazoezi wanafanyia wake zao au’.
Katika kesi
nyingine, mshtakiwa Juma Mtatuu akiwa eneo la Ocean Road, Agosti 24, mwaka huu
anadaiwa kuwa alituma ujumbe katika Facebook akisema ‘Huyu hata akifa ataenda peponi, na kufanya mazoezi kote kule wamekufa
Mbagala, mimi nitakuwa wa kwanza kuandamana kule Kahama, tarehe moja
naelekea Kahama kwa Ukuta, mimi nitakuwa namba moja kushika bendera ya Ukuta,
kifo kipo tuu, usiogope kwani mawe na mapanga yameisha’
No comments:
Post a Comment