
Kompyuta mpakato zenye majibu ya
watu waliopima ukimwi pamoja na majina yao zimeibwa mkoani Tabora.
Kompyuta hizo zipatazo 30 zenye
thamani ya Sh70 milioni, zimeibwa kwenye ofisi ya shirika lisilo la kiserikali
la Jhpiego linaloshughulika na masuala ya Ukimwi na tohara.
Kompyuta hizo zimeibwa mwishoni mwa
wiki kwenye ofisi hiyo iliyo jirani na ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa (Takukuru).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora,
Hamis Issa amesema tayari taarifa za tukio hilo zimewafikia na
wanaendelea na uchunguzi wa kina kufahamu kilichotokea.
Inadaiwa kuwa kompyuta hizo, zina
majina ya watu waliopima VVU na majibu yao.
“Kinachotatiza ni kwamba kama
majina ya watu wenye virusi yakijulikana itakuwa ni utata mkubwa kwani ofisi
hiyo itakuwa imewaweka katika wakati mgumu pasipo wao kupenda,” kilisema chanzo
chetu cha habari.
Mkurugenzi wa Jhipego, Dk Albert
Komba amethibitisha kutokea kwa wizi huo.
No comments:
Post a Comment