Kama unataka
ushangazwe na maajabu ya dunia, basi kitabu cha Guinness World Records hakina
mpinzani. Kimesheheni mambo, watu, vitu na vingine vinavyoweza kukuacha mdomo
wazi.
Mwanamke mwenye umri mdogo
aliye na ndevu nyingi: Harnaam Kaur wa Uingereza, ana ndevu zenye urefu inchi
sita. Ana umri wa miaka 24
Kitabu
kipya, toleo la 62 kwaajili ya mwaka 2017 kimetoka kikiwa na maajabu zaidi ya
4,000. Kitabu hicho kimeingia sokoni Alhamis hii na kinauzwa kwa £20. Haya ni
baadhi ya maajabu yaliyomo kwenye kitabu hicho kipya.
Paka mrefu
zaidi: Akiwa na urefu wa futi 3ft 10.6in, Ludo anaishi na mmiliki wake Kelsey
Gill huko Ryhill, West Yorkshire. Anasema: ‘Ni rafiki wa wote lakini baadhi ya
wageni humuogopa sababu wamezoea kuona mbwa mwenye ukubwa kama wake’
Maxwell Day,
14, anaweza kuizungusha miguu yake kwa nyuzi 157
Mbwa mwenye
mkia mrefu zaidi: Keon ana mkia wenye urefu wa inchi 30.2. Anaishi Ubelgiji
Mtu aliyevutwa
na farasi umbali mrefu zaidi akiwa amewashwa moto. Josef Todtling wa Austria,
alivutwa umbali wa futi 1,640 akiwa amewashwa moto mwili mzima. Alikuwa amevaa
nguo nyingi. Ameshikilia rekodi kwa kutumia dakika 4 na sekunde 41
Domo Kubwa:
Bernd Schmidt, 47, wa Wendlingen, Ujerumani anaweza kuufungua mdomo wake kwa
upana wa inchi 3.46
Mabonge ya ice
cream yaliyopangwa kwa wiki bila kuanguka. Rekodi hii inashikiliwa na Dimitri
Panciera, 54 wa Italia. Alirundika mabonge 121
Mbwa jike
mrefu kuliko wote duniani. Dane Lizzy, ana urefu wa inchi 37.96 na anaishi
Alva, Florida, Marekani
Mkusanyiko
mkubwa zaidi wa vitu vinavyohusiana na hamburger. Harry Sperl (aka Hamburger
Harry) kutoka Ujerumani amekusanya vitu 3,724
Mtu mwenye
umri mkubwa mwenye tattoo nyingi zaidi: Ms Guttenberg, 67 amejichora asilimia
91.5 yake mwili wake
Chanzo: Mail Online
Chanzo: Mail Online
No comments:
Post a Comment