
Baraza la Wazee wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) limetoa pongezi kwa Kamati Kuu ya chama hicho
kuahirisha maandamano na mikutano ya nchi nzima iliyopewa jina la Ukuta.
Maandamano hayo ambayo yalipangwa
kufanyika kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu yaliahirishwa na Kamati Kuu ya chama
hicho kwa madai ya kuombwa na viongozi wakuu wa madhehebu ya dini.
Akizungumza katika Makao Makuu ya
chama hicho jana, Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Roderick Lutembeka alisema, hatua
ya kamati hiyo kuahirisha maandamano hayo ni muhimu na inaonesha jinsi chama
hicho kina viongozi wavumilivu.
“Kwa kutambua moyo wa kiuongozi
waliouonesha na dhamira ya dhati ya kuwatumikia Watanzania wote, tunapenda
kuwapongeza viongozi wetu wakuu kwa uamuzi huu wa busara ambao umeuthibitishia
umma kuwa chama kina viongozi imara,” alisema Lutembeka
Katika hatua nyingine, baraza hilo
limesema limebaini kuwepo kwa njama zinazopikwa dhidi ya chama hicho kupitia
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Baraza la Vyama vya Siasa nchini,
kukifuta chama hicho.
“Taarifa zinaonesha njama hizo
zinalenga kukihujumu Chadema kwa kuandaa mitego haramu ya kisiasa ili hatimaye
yatolewe mapendekezo ya kukifuta katika orodha ya vyama vya siasa,” alisema
Lutembeka na kuongeza;
“Tarehe 15 Agosti mwaka huu Jaji
Mtungi alitangaza kuwa, Baraza la Vyama vya Siasa lilikuwa limeitisha kikao
ambacho kingefanyika tarehe 29-30 Agosti kujadili masuala ya hali ya kisiasa
nchini. Siku mbili kabla ya kikao Mwenyekiti wa baraza akatangaza kukiahirisha
hadi tarehe 3-4 mwezi huu.
“Jambo la kushangaza baada ya
busara kutumika kupitia viongozi wa dini kushawishi Chadema kuahirisha kwa
kutoa mwanya wa mazungumzo hadi tarehe 1 mwezi ujao, Kamati ya Uongozi wa
Baraza la Vyama vya Siasa ikaibuka tena na kutangaza kuahirisha kikao cha
baraza hadi itakapotangazwa tena.
“Wakati taarifa zote hizo
zikitolewa na viongozi wa baraza, ofisini hapa (Chadema) hakuna hata barua moja
kutoka kwa msajili ya kutuita katika kikao chochote kati ya hivyo. Kuanzia kile
cha tarehe 29-30 Agosti, tarehe 3-4 Septemba wala hiyo ya kuahirisha.
“Katika mazingira haya nani ambaye
hatashawishika kuamini ofisi ya msajili inatii maagizo ya watawala,”
No comments:
Post a Comment