ZINGATIA HAYA KABLA YA KUFUNGA NDOA - OREST NGOWI

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Wednesday, 21 September 2016

ZINGATIA HAYA KABLA YA KUFUNGA NDOA

Responsive Ads Here
   husband-and-wife1
Hii si tuu kwa mahusiano ya kimapenzi,bali hata dini zinafundisha kuwa Mungu anapenda na katika hilo, hakuna budi ya kutii amri zake, na kwamba ikifanyika vinginevyo maana ya upendo inakuwa imepotea.


Fedha:  Katika swala la fedha, jambo kubwa linalojitokeza ni namna ya kufanya maamuzi kuhusu matumizi ya fedha, Ni muhimu kuweka mikakati
ya pamoja kwa mambo ya msingi kimaisha na kila mmoja kutilia maanani mipango hiyo, kabla ya kuamua kutumia kipato chake kwa mambo ambayo pengine hayapo nje ya mipango ya kifedha ya wawili nyie kama wapenzi.

Imani: Katika swala la imani ni muhimu kufahamiana vyema mwenendo wa kiimani wa mwenza wako, na kuheshimu kuwa swala hili ni nyeti, na mabadiliko ya kweli hayawezi kulazimishwa,Imani inaweza athiri namna mnavyoweza kuwasiliana kama wapenzi,kwani mwingine mwenye msimamo mkali wa kidini, anaweza kukataa jambo fulani hapo baadae, jambo ambalo pengine mwenza wake anaona ni jambo la kawaida tuu

Mahali pa kuish
i:  Mtaa gani,wilaya gani,mkoani gani, nchi gani au bara gani kila mmoja wenu anatazamia muishi ni jambo la msingi kuliweka wazi kati yenu. Jambo hili linaweza kuendana na mambo mengine
mengi ambayo yanachochea mabadiliko ya muda mfupi na hata muda mrefu katika maisha yenu, kama vile aina ya kazi mnazotarajia kila mmoja wenu kufanya, na aina ya kazi unazotamani au kufikiri ni vema mwenza
wako afanye.

Watoto: 
Hili ni jambo zito haswa katika vipengele vya lini watoto wapatikane (ujauzito), idadi ya watoto, aina ya malezi kwa watoto watakao patikana, na zaidi sana majukumu ya kifedha katika malezi ya watoto (mfano, nani atalipa ada ya shule, n.k). Pamoja na kutafakari
hayo, watu wawili mlio katika mahusiano, ni muhimu mkatengeneza picha ya maisha ya watoto wenu endapo mmoja wenu atatangulia mbele za haki.

Hisia za kimapenzi:
 Ni jambo la msingi kutokupuuzia hisia za kimapenzi za kila mmoja wenu, yakupasa kutambua vile mwenzako angependa akuone unamvutia na vile ambavyo unamjali hisia zake.

Ni kweli kuwa katika mahusiano,hisia za kimapenzi zinaweza zisichukue nafasi kubwa kati yenu kwani
kuna mambo mengi ya kufanya pamoja kama wapenzi, hata hivyo pamoja na udogo wake wa muda, jambo hili nyeti lisipopewa kipaumbele, linaweza sababisha mengine yote kuharibika.


kweli ni kuwa watu wawili wanapoamua kwa dhati kuwa katika mahusiano ni kwamba wanakuwa tayari huku katika akili zao wanakuwa wamejenga matarajio au matumaini ya kunufaika na uhusiano husika, hata kama hawawezi kuambiana moja kwa moja.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad