Kiungo huyo wa kati wa England alifunga bao la kwanza dakika ya
33.
Reading karibu wasawazishe baada ya mpira wakupinduliwa, wake
Callum Harriott kutua juu ya lango lililokuwa linalindwa na Emiliano Martinez.
Arsenal walitawala mechi kipindi cha pili na Oxlade-Chamberlain
akaongeza bao la pili dakika ya 78 na kuwawezesha kumaliza mechi ya 14 bila
kushindwa.
Oxlade-Chamberlain, 23, alikuwa amesumbuka kupata nafasi kikosi
cha kwanza timu ya Arsene Wenger mapema msimu huu.
Amecheza dakika 90 mechi mbili pekee, lakini kutokana na
uchezaji wake mzuri karibuni, amempatia Wenger kila sababu ya kumpa nafasi
kikosini.
Matokeo ya mechi
za EFL
§
Arsenal 2-0 Reading
§
Bristol City 1-2 Hull
§
Leeds 2-2 Norwich
§
(Leeds United wakashinda 3-2 kupitia penalti)
§
Liverpool 2-1 Tottenham
§
Newcastle 6-0 Preston
No comments:
Post a Comment