Bondia,
Francis Miyeyusho aliyekuwa mwanafunzi wake, ameiambia East Africa Radio kuwa
Mashali aliumizwa vibaya kichwani. Amesema Jumapili hadi saa tisa alasiri
walikuwa pamoja kwenye kikao cha masuala ya masumbwi na alimuaga kuwa anaenda
Kimara.
“Baadaye nikaja kusikia story
kwamba kuna mtu kagombana naye pale wamemchenjia wameanza kumuitia kelele za
mwizi mitaa ya Kimara huko kwahiyo wamemchangia raia, wamempiga,” amesimulia
Miyeyusho.
Bondia huyo amesema kuwa Mashali alikuwa
amenyoa rasta zake na kwamba huenda hiyo ni sababu wananchi wengi walishindwa
kumtambua.
Kwa
upande wa baba yake mzazi, Mzee Christopher Mashali, amesema alipata taarifa
hizo usiku akiwa amelala kutoka kwa vijana wanaomfahamu. Vijana hao walimweleza
kuwa mtoto wake amepigwa vibaya kiasi cha kupasuliwa kichwa na usiku huo
kuwapigia simu wanae wengine waliopo Dar.
Anasema Mashali alifariki Muhimbili
kutokana na kuwa amejeruhiwa mno ikiwa ni pamoja na kutolewa ubongo. Mzee
Mashali anasema mara ya mwisho kuwasiliana na mwanae ilikuwa jana (Jumapili)
mchana.
“Alinitumia meseji ambayo bado
ninayo hapa akaniambia ‘baba nipo kwenye kikao, nikimaliza kikao nitakujibu
baba’ ndio mara ya mwisho nimewasiliana naye,” ameeleza mzee huyo.
Amesema kinachoendelea sasa ni
kupata ripoti ya polisi, kupewa ruhusa ya kuuchukua mwili wa marehemu tayari
kwa mazishi.
Mashali aliyezaliwa mwaka 1980,
ameacha watoto watano.
No comments:
Post a Comment