Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, William Lukuvi, ameeleza
jinsi matapeli wa ardhi wanavyoshirikiana na baadhi ya maafisa ardhi hasa wa
halmashauri za manispaa na jiji kutekeleza utapeli wa ardhi kwa kutumia barua
bandia.
Lukuvi
ameeleza hayo wakati akihojiwa katika kipindi cha ‘KUMEKUCHA’ kinachorushwa na
kituo cha runinga cha ITV.
“Mtu akinunua ardhi hupewa karatasi
za ofa ambazo hivi sasa zilizojaa ni feki, lakini wapo wajanja na matapeli
wanatumia ofa hizo kudhulumu viwanja vilivyo wazi. Mfano wakiona kiwanja kipo
wazi wanakwenda katika halmashauri wanashirikiana na baadhi ya maafisa ardhi wasio
waaminifu, wanauliza namba ya ploti ya kiwanja husika na anayemiliki,” alisema.
“Wakishajua namba na mmiliki wa
kiwanja huiondoa ofa halali katika faili kisha afisa ardhi anaiweka feki, siku
mmiliki halali akienda kuulizia kiwanja chake katika halmashauri anakuta ofa
yake haipo ipo ya mtu mwingine ambaye ameghushi tarehe ya barua ya
ofa,”aliongeza.
Aidha Lukuvi alisema matapeli wa
ardhi huyafahamu maeneo yaliyo wazi na kwamba asilimia kubwa hushughulika na
yale ambayo wamiliki wake wamefariki dunia.
“Hawa matapeli huyajua maeneo
vizuri, na wanachokifanya ni kutengeneza ofa feki kisha kuziweka katika faili
za halmashauri, ukienda mmiliki halali unaambiwa ni tapeli kwa kuwa barua yako
haiko katika faili,” amesema na kuongeza,”Matapeli wanaishi mjini kwa kutengeneza
ofa bandia, wastaafu,yatima na wajane wanalizwa kila siku,” amesema.
Ametoa agizo kwa maafisa ardhi wa
kanda kutotoa huduma wala kushugulika na barua za ofa kwa sababu baadhi yao
ndio wanaobadilisha ofa halali za watu.
BY: EMMY MWAIPOPO
No comments:
Post a Comment