Ametoa
kauli hiyo alipokutana na waziri mkuu, Kassim Majaliwa jijini Dar es Salaam.
Bakhresa amesema ana mpango wa kujenga kiwanda kimoja kwenye mikoa ya kanda ya
ziwa na kwamba wamefikia uamuzi huo baada ya kuona kuwa watu wanapata usumbufu
wa kuisafirisha matunda hadi Dar es salaam kwaajili ya soko.
Kwa upande wake wake waziri mkuu
amemhakikishia kwamba nia ya serikali ya awamu ya tano ni kushirikiana na
wafanya biashara na wamiliki wa viwanda kutokana na dhamira ya kukuza uchumi wa
Tanzania kupitia uzalishaji wa viwandani na kumtaka mfanya biashara huyo
kuangalia maeneo mengine ya kuwekeza kwenye sekta za hoteli na utalii ili
kukuza uchumi wa nchi.
Kampuni hiyo yenye matawi Rwanda,
Burundi,Msumbiji,Malawi,Zimbabwe na Afrika ya Kusini inatengeneza vyakula
mbalimbali ikiwemo juice,soda, maji,biscuit,ice cream,vyakula vya nafaka vya
ngano,mahindi,mchele na bidhaa za kuokwa.
BY:EMMY MWAIPOPO

No comments:
Post a Comment