Serikali imesema uhakiki wa watumishi wa umma, utakamilika ndani ya
mwezi huu, hivyo nafasi zilizoachwa wazi baada ya kuondolewa kwa watumishi
hewa, zitaanza kujazwa.
Akizungumza
katika awamu ya pili ya kipindi cha ‘Tunatekeleza’ kinachorushwa TBC 1 , katibu
mkuu ofisi ya rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Laurean
Ndumbaro alisema uhakiki wa watumishi hewa, umesaidia kuongeza ufanisi katika
taasisi zake.
“Kwa mfano, yupo mtu anatumia
majina matatu lakini akatokea mmoja akaondoa lile la katikati na kubaki na
majina mawili labda Laurean Ndumbaro hivyo mfumo utaona kuwa ni jina jipya
kumbe kuna mtu ambaye amejitengenezea jina hilo,” alisema Dk Ndumbaro.
“Kauli ya Rais ya ‘Hapa Kazi Tu’
inatekelezwa vizuri katika utumishi wa umma. Majukumu yetu ni kuandaa na
kusimamia sera, kanuni, taratibu, sheria miundo na miongozo inayohusu
rasilimali watu katika watumishi wa umma. Pia jukumu la kusimamia maadili ya
utumishi wa umma hasa wale ambao hawaangukii kwenye tume ya maadili ambao sio
viongozi wa juu,’’ alifafanua.
Aidha, imesema kwamba baada ya
uhakiki huo ambao utasaidia kuwa na orodha sahihi ya watumishi waliopo katika
taasisi za umma kwa lengo la kuboresha hali ya utumishi nchini, itaanza mfumo
wa kuhakiki majina mapya.
BY: EMMY MWAIPOPO

No comments:
Post a Comment