Rapper Bill Nas anatuhumiwa kutumia verse za wimbo wa msanii
chipukizi ambaye amefanya cover ya ‘Pana’ Chris Roby kwenye wimbo wa Nuh
Mziwanda.
Muimbaji
huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio kuwa Bill alitoa
verse aliyoweka kwenye wimbo wake na kuhamishia kwenye wimbo wa Nuh.
“Bill Nas alikuwa mshikaji wangu
tangu siku nyingi, tulifanya nyimbo wakati akiwa na wimbo wake wa ‘Ligi Ndogo’.
Baada ya muda Bill Nas kuona wimbo nachelewesha kuutoa akahamishia verse yake
kwenye wimbo wa Nuh Mziwanda ambao bado haujatoka lakini tayari wameshafanya
mpaka video,” amesema Chris.
“Wakati ambao mimi nilikuwa nataka
kuuachia wimbo huo nilimpigia simu nahitaji support yake aliniambia nisiuachie
kwa kuwa tayari verse kashahamishia kwenye wimbo wa Nuh. Nikaamua kuachana na project
hiyo nikaamua kufanya cover ya wimbo huu wa ‘Pana’.”
Akijibu tuhuma hizo Bill Nas
ameiambia Bongo5 kuwa hamfahamu kabisa msanii huyo na wala hajawahi kumsikia.
Cover version ya wimbo wa ‘Pana’ ulioimbwa na Chris Roby ni moja kati ya cover
kali zilizowahi kuimbwa na baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva.
No comments:
Post a Comment