Kuna model maarufu wa Bongo aliyetosa kuonekana kwenye video
ya wimbo wa Diamond ‘Salome.’
Model
huyo anadaiwa kutaka alipwe fedha nyingi ambazo zilikuwa nje ya bajeti ya staa
huyo.
“Bajeti yangu haikuweza kumuafford,
na siwezi kufanya kitu kimashauzi wakati bajeti yangu ndogo,” Diamond
alikiambia kipindi cha The Playlist cha Times.
Diamond
anasema alichokikosa model huyo baada ya kukataa kufanya video hiyo si fedha
tu, bali exposure ambayo angeipata baada ya hapo.
“Si uchawi, sio uongo, sio
ushirikina, unavyofanya video na mimi unakuwa mkubwa na inakuongezea dau,”
alisisitiza kwa kuongeza kuwa watu kibao humuomba waonekane kwenye video zake
bure lakini hukataa kwakuwa ni lazima awalipe.
Diamond amedai hiyo ndio sababu
hatokuja kulitaja jina lake kwakuwa atampa kiki na atakuwa mkubwa.
“Nilimuambia, angalia angle zote
mbili, angalia kwamba nakulipa kiasi lakini kushiriki kwako kwenye hii video
itakuongezea ukubwa zaidi, itakupa biashara nyingi.”
Alitoa mfano kuwa show nyingi za
MTV alizowahi kutumbuiza alifanya bure kwasababu alizitumia kukuza jina lake.
Anasema wakati mwingine hadi dancers huwasafirisha kwa gharama zake mwenyewe.
“Lakini najua show ninayoifanya
pale ikitoka itanipa hela nyingi baadaye. Niliheshimu alichokisema ndio maana
sikumind, nilisema naheshimu sababu umejitambua na umeona thamani yako ni nini,
lakini bahati mbaya sisi bajeti yetu haikufika huko.”
No comments:
Post a Comment