Serikali ya Burundi imechukua
uamuzi wa kusitisha ushirikiano wake na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za
Binadamu, inayotuhumiwa kula njama katika kuandaa ripoti ya Uchunguzi Huru wa
Umoja wa Mataifa (EINUB).
"Kufuatia njama ya Ofisi ya
Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu nchini Burundi, katika maandalizi ya ripoti
ya uongo na yenye utata ya Wataalam wanaodaiwa kufanya Uchunguzi Huru wa Umoja
wa Mataifa nchini Burundi (EINUB), Serikali ya Burundi imeamua kusitisha
ushirikiano wowote na kushirikiana katika miundo yake yote, pamoja na Ofisi ya
Umoja wa Mataifa ya Haki za Binanadamu hadi itakapotangazwa tena." Maneno haya
yameonekana kwenye tangazo lililosainiwa Jumanne hii Oktoba 11, 2016 na
Philippe Nzobonariba, katibu Dola na Msemaji wa serikali.
Kwa mujibu wa tangazo hili, uamuzi
huo ulifahamishwa maofisa wa Ofisi hii wakati wa kikao cha kazi pamoja na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Burundi Alain Aimé
Nyamitwe, Jumatatu hii, Oktoba 10, 2016.
"Kwa maana hii, Burundi
inaomba kwa kusubiri, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu kuteua timu
itakayoendesha mazungumzo kuhusu makubaliano ya makao makuu, ambayo yataweka
wazi majukumu yake, muda na idadi ya wafanyakazi wake nchini Burundi,"imeongeza taarifa
hiyo.
Uamuzi huu unakuja baada ya
maandamano mjini Bujumbura mwishoni mwa wiki iliyopita mbele ya makao makuu ya
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu ambapo waandamanaji waliomba
ofisi hiyo kufungwa haraka iwezekanavyo.
Ripoti ya EINUB ilikuwa chanzo cha
azimio HRC33 lililochukuliwa na Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu
ambalo linaomba kuundwa kwa Tume ya Kimataifa ya Uchunguzi wa ukiukaji wa haki
zabinadammu nchini Burundi.Azimio ambalo lilikataliwa na serikali ya Burundi,
ambayo inautuhumu Umoja wa Ulaya kuwa imeandaa na kupanga njama dhidi yake.
No comments:
Post a Comment