Amesema Marekani inafaa kuangazia zaidi kushinda vita dhidi ya
kundi linalojiita Islamic State badala ya kulenga kumshawishi au kumshinikiza
Rais wa Syria Bashar al-Assad kung'atuka uongozini.
Bi Clinton amekuwa akipendekeza kutolewe marufuku ya ndege
kutopaa katika anga ya Syria, mpango ambao baadhi wanasema huenda ukasababisha
mgogoro na ndege za kivita za Urusi ambazo zinatekeleza mashambulio dhidi ya
waasi wanaompinga Bw Assad.
Maafisa wa kampeni wa Bi Clinton wamemtuhumu Bw Trump kwa
"kuwachezea Wamarekani kupitia wasiwasi wao".
Bw Trump pia amewashambulia wafuasi na viongozi wa Republican
ambao wamekataa kumuunga mkono.
"Iwapo tungekuwa na umoja, hatungeshindwa na Hillary
Clinton kwenye uchaguzi huu," aliambia shirika la habari la Reuters katika
uwanja wa gofu wa Trump National Doral mjini Miami, Florida.
Mgombea huyo ametishia kwamba hali mbaya zaidi itatokea iwapo
mpango wa mpinzani wake wa chama cha Democratic wa kutaka kudhibiti anga ya
Syria utatekelezwa.
"Mtajipata katika Vita Vikuu vya Tatu vya Dunia huko Syria
iwapo tutamsikiliza Hillary Clinton," Bw Trump amesema.
"Hampigani tena dhidi ya Syria, mnapigana na Syria, Urusi
na Iran, mnafahamu?
"Urusi ni taifa lenye uwezo wa kinyuklia, lakini taifa
ambalo silaha zake za nyuklia hufanya kazi kinyume na nchi nyingine ambazo kwao
ni maneno tu."
Amedokeza kuwa Bi Clinton hataweza kufanya mazungumzo na Rais wa
Urusi Vladimir Putin ikizingatiwa kwamba amekuwa akimshutumu sana kiongozi huyo
kwenye kampeni.
Bw Trump ameshangaa: "Ataenda vipi na kufanya mazungumzo na
mtu ambaye amemuonyesha kuwa ni mtu mwovu sana?" iwapo atachaguliwa kuwa
rais tarehe 8 Novemba.
Maafisa wa kampeni wa Bi Clinton hata hivyo wamepuuzilia mbali
ukosoaji huo na kusema wataalamu wa usalama wa taifa wa Republican na
Democratic wamemshutumu Bw Trump na kusema hafai kuwa amiri jeshi mkuu.
"Kwa mara nyingine, anazungumza kama kasuku kumhusu Putin
na kuchezea wasiwasi wa Wamarekani, lakini anakataa kusema mipango yake ya
kuwashinda ISIS au kumaliza mzozo wa kibinadamu nchini Syria," msemaji wa
Bi Clinton, Jesse Lehrich amesema kupitia taarifa.
Tahadhari hiyo kutoka kwa Bw Trump ni sawa na tahadhari
iliyotolewa na afisa mkuu wa jeshi la Marekani katika kikao cha wabunge.
Mwenyekiri wa majeshi ya pamoja Jenerali Joseph Dunford aliambia
wabunge kuwa kutangaza marufuku ya kuzuia ndege kupaa anga ya Syria kunaweza
kusababishwa vita na Syria.
"Kwa sasa, seneta, ndipo tuweze kudhibiti anga yote ya
Syria, itatuhitaji kwenda vitani na Syria na Urusi," Jenerali Dunford
aliambia kamati ya huduma za jeshi katika seneti.
"Huo bila shaka ni uamuzi ambao sitachukua."
Kwenye mdahalo wa mwisho wa urais Nevada 20 Oktoba, Bi Clinton
alieleza uungaji mkono wake kwa hatua hiyo.
"Marufuku ya ndege kutopaa inaweza kuokoa maisha na
kuharakisha mwisho wa mzozo huo," alisema.
Lakini mwaka 2013, kwenye hotuba kikao cha Goldman Sachs, Bi
Clinton alikuwa amesema marufuku kama hiyo inaweza "kuwaua watu wengi wa
Syria", kwa mujibu wa maandishi ya hotuba hiyo yaliyofichuliwa na
Wikileaks.
Vifo vya raia vinaweza kutokana na haja ya wanajeshi wa Marekani
kushambulia ngome za wanajeshi wa Syria ambazo zimo maeneo yenye raia wengi.
Wagombea
wanatarajiwa kutumia siku 14 zilizosalia kujipigia debe. Wanatarajiwa kupiga
kampeni sana majimbo yanayoshindaniwa kama vile Ohio, Carolina Kaskazini,
Florida na Pennsylvania
Uchaguzi utafanyika Jumanne 8 Novemba kuamua Rais wa 45 wa
Marekani.
Rais mpya ataapishwa 20 Januari 2017
No comments:
Post a Comment