Ni siku chache tu zimepita baada ya kushuhudia utambulisho wa label mpya
ya muziki, Ndauka Music inayomilikiwa Rose Ndauka.
Uzinduzi wa label hiyo
ulienda sambamba na kutambulishwa kwa msanii wake mpya Casso, sambamba na wimbo
wake, Kitonga ambao umeshaanza kuchezwa kwenye redio na TV.
Baada
ya utambulisho huo kupita hatimaye Rose Ndauka amesema mpaka sasa ameshatumia
takriban shilingi milioni 20 kuisimamisha Ndauka Music.
“Mpaka hapo ilipofikia
approximately nimeshatumia kama milioni 20 na.. mpaka hapa nilipofikia lakini
sio kwamba hiyo ndio itakayowezesha Ndauka Music kusimama, bado tunaendelea
kuinvest,” amesema Ndauka nilipofanya naye mahojiano ofisini kwake Mwenge.
Ujio wa Ndauka music unazidi
kuongeza idadi ya music label hapa nchini ikitanguliwa na label kadhaa kama
Tiptop Connection, Mkubwa na Wanawe, LFLG, Endless Fame, WCB, The Industry za
zingine.
BY EDWARD FABIAN
No comments:
Post a Comment