
Usitarajie kabisa kusikia collabo ya Vanessa Mdee na msanii wa Marekani
siku za hivi karibuni.
Muimbaji
huyo wa Juu, amesema muda wa kufanya hivyo kwake bado haujafika. “Nadhani
nitawafaidisha zaidi wao zaidi ya wao kunifaidisha mimi,” Vanessa alisema
Jumatano hii kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.
“Because hawatafanya promo ya wimbo
wetu Marekani but mimi nitafanya promo ya wimbo wao huku Afrika,” aliongeza.
“So I want to get to a point where kama vile Wizkid alivyofanya One Dance
imewafaidisha wote wawili. So bado hatujafikia hatua ya kusema kwamba now I am
going to work with, na tutafanya equal promo, haipo! What is it for kama wote
hamfikii mashabiki wa wenzako, it doesn’t make any sense.”
Vanessa alitolea mfano wimbo wa
Davido aliomshirikisha Meek Mill ‘Fans Mi’ ambao msanii huyo wa Marekani hakuwahi
kusema chochote.
“Meek hata kupost kicover hajapost,
so what is it for na amelipwa hela nyingi sana, I don’t know if we can do
that,” alisisitiza.
Watangazaji wa kipindi hicho nao
waliyaunga mkono mawazo ya Vanessa.

No comments:
Post a Comment