
Msanii wa muziki kutoka WCB, Raymond ‘Rayvanny’ amefunguka kwa kusema
kuwa msanii akiwa chini ya label ya WCB hakatazwi kuanzisha label yake na
kusimamia wasanii.
Muimbaji
huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Natafuta Kiki’, Jumatano hii amekiambia
kipindi cha Uhurufleva kinachoruka Uhuru FM kuwa kwa hatua aliyofikia hashindwi
kuanzisha label ya kumsimamia wasanii.
“Kila kitu kwenye maisha kinatokea
kwa sababu, na katika maisha lazima uwe na mipango. Unajua alichokifanya
Diamond pamoja na team yake, Mkubwa Fella, Babu Tale pamoja na Sallam ni kitu
kikubwa sana,” alisema Rayvanny “Lakini kuwa na wasanii wangu pamoja na label
hayo mambo yanawezekana, WCB haimzuii mtu,”
Aliongeza, “Naweza nikawa na WCB na
nikawa na label yangu lakini lazima niangalie. Tunamuona Kanye West yupo kwa
Jay Z lakini ana wasanii wake na vyote amefanya kutokana na nafasi yake. Kwa
hapa nilipo sishindwi kumsimamia msanii, kumlipia video, kumlipia audio. Pia
sishindwi kumfanyia msanii promotion, lakini nikisema nimchukue msanii
nimsimamie sasa hivi nitafika sehemu tu nitanasa, kwa sababu kumsimamia msanii
sio tu kumlipia video na audio, kuna mambo mengi,”
Pia muimbaji huyo amesema wimbo
‘Salome’ aliyoshirikishwa na Diamond ni wimbo ambao umemtangaza zaidi kuliko
nyimbo zake za nyuma.

No comments:
Post a Comment