Manowari hiyo ya Marekani
ilishambuliwa ikiwa maeneo ya bahari ya kimataifa.
Pentagon imesema tathmini ya awali
inaonesha maeneo matatu yenye mitambo ya rada, ambayo yanashukiwa kutumiwa
kutekeleza mashambulio hayo, yameharibiwa.
Jeshi hilo la Marekani limesema
maeneo yaliyoshambuliwa yanamilikiwa na waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na
Iran.
Pentagon imesema mashambulio hayo
ya makombora yaliidhinishwa na Rais Obama, na yalitekelezwa kulinda manowari za
Marekani na wanajeshi wake na pia kuhakikisha uhuru wa watu wanaopitia Bahari
ya Sham kwenye ufuo wa Yemen.
Mashambulio hayo yalitekelezwa kwa
makombora ya Tomahawk yaliyofyatuliwa kutoka kwa manowari ya USS Nitze.

No comments:
Post a Comment