Dayna Nyange amefunguka kuwa atakuwa tayari kuwa chini ya lebo
yoyote endapo watakubaliana na masharti yake.
Hitmaker huyo wa ‘Komela’ amemuambia mtangazaji wa
Maisha FM ya Dodoma, Silver Touchez “Kikubwa nachoangalia ni sababu, kabla
sijajiunga na lebo yoyote lazima niwe na vitu vyangu ambavyo navitaka na wao
wanavitu vyao wanavyotaka.”
“Record label ni studio tu ambao
watu watakuwa wanasimamia kazi zangu ni kitu ambacho mimi mwenyewe ninaweza
nikaenda sehemu yoyote nikafanya kazi zangu. Kuna vitu vingi sana kabla
hujaingia kwenye lebo yoyote kama kuna makubaliano mazuri yatakuwepo basi tutafanya
kazi,” ameongeza.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo
amekanusha kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na Idris Sultan zaidi ya kuwa
marafiki tu.
No comments:
Post a Comment