Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe January Makamba ameendelea na ziara yake katika
Mkoa wa Katavi kwa kutembelea kijiji cha Kabege ambapo aliangalia mradi Mkubwa
wa Umwagiliaji wa Mwamkulu katika Manispaa ya Mpanda ambao kwasasa umesitisha
kutoa huduma zake kwa kukosekana kwa maji ya kutosha katika Mto Katuma.
Katika kikao cha Majumuisho ya
Ziara yake ya siku mbili katika Mkoa wa Katavi, Waziri Makamba ameutaka uongozi
wa Mkoa huo kudhibiti yafuatayo:
1. Ongezeko la watu na mifugo
ambayo kwa kiasi kikubwa inachangia uharibifu wa mazingira.
2. Kusitisha uchepushaji kwa Mto
Katuma ambapo taarifa ya Mkoa ilieleza kuna jumla yamabanio 40 ambayo
yanatumiwa na watu kuchepusha maji kwa ajili ya manufaa yao binafsi.
3. Uchimbaji hatari wa Madini
usiofuata taratibu
4. Kuhuisha sheria ndogo ndogo za
mazingira katika ngazi mbalimbali za Serikali za mitaa
5. Kuanisha maeneo maalumu ambayo
yatatangazwa katika Gazeti la Serikali kama mazingiranyeti ili kuyapa ulinzi
zaidi
6. Kusimamia uondoshwaji wa
wavamizi katika Vyanzo vya maji
7. Kufanyika kwa sensa ya mifugo ili
kujua Mkoa una mifugo kiasi gani na kubuni namna boraya kuhumudimia mifugo hiyo
bila kuathiri mazingira
8. Ameahidi kuaanda andiko maalumu
la Mradi wa Ziwa Katuma
9. Mmiliki wa Jema Sitalike Project
kutafutwa popote alipo, leseni yake ya madini isitishwe,apigwe faini na
kurekebisha eneo alilokuwa akitumia awali kwa shughuli za uchenjuaji wadhahabu.
10. Waziri Makamba meagiza
Watendaji kata na Vijiji kutotoa vibali vya uchimbaji wa madini bila kufuata
utaratimu wa Wizara ya Nishati na Madini.
Aidha Waziri Makamba amewasili
Katika Mkoa wa Kigoma na kutembelea kiwanda cha Nyanza Mines nakuwapongeza kwa
kuzalisha chumvi kwa kutumia nishati ya jua ambapo awali kiwanda hicho
kilifungiwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kutokana
na uharibifu wa Mazingira kwa kutumia magogo mengi mwaka 2015. Kiwanda hicho
kwa sasa kinazalisha tani 20,000-25,000 ndani ya miezi mitatu.
No comments:
Post a Comment