Reli hiyo imejengwa na kampuni mbili za Uchina, kwa gharama ya
takriban dola 4 bilioni za Kimarekani ambazo zilitolewa na serikali ya Uchina
kama mkopo.
Reli hiyo inatarajiwa kuipa Ethiopia njia rahisi ya kufikisha
bidhaa zake, hasa mazao ya kilimo, hadi dandarini.
Uchumi wa Ethiopia umekuwa ukikua kwa kasi kutokana na ongezeko
la uzalishaj wa kilimo na ukuaji pia wa miji.
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, Ethiopia, yenye watu 97 milioni ni
moja ya mataifa yenye uchumi unaokua kwa kasi zaidi duniani kwa sasa.
Kwa mujibu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, uchumi wa taifa hilo
ulikua kwa asilimia 10.2 mwaka 2014/15, na kasi hiyo inatarajiwa kuendelea
mwaka 2016 na mwaka 2017.
Reli hiyo ni ya umbali wakilomita 752, na kasi yake ya wastani
itakuwa kilomita 120 kwa saa, jambo litakalofupisha safari ya kutoka Addis
Ababa hadi Djibouti kuwa chini ya saa kumi ikilinganishwa na siku mbili
zilizotumiwa awali.
Reli hiyo ndio mradi wa pili mkubwa wa reli inayounganisha
mataifa zaidi ya mawili ambayo imejengwa na kampuni za Kichina barani Afrika.
Mradi huo mwingine ni reli ya Tazara inayounganisha jiji la Dar
es Salaam, Tanzania na mji wa Kapiri Mposhi nchini Zambia.
Wakati wa ziara yake Ethiopia Mei 2013, naibu waziri mkuu wa
China Wang Yang alisema mradi huo wa reli wa Ethiopia-Djibouti ni "Tazara
ya enzi mpya."
Kinyume na mradi wa Tazara, ambao ulijengwa miaka ya 1970 kama
mradi wa msaada wa kimataifa kutoka kwa serikali ya Uchina, reli hiyo ya
Ethiopia-Djibouti ni mradi wa kibiashara kati ya kampuni za Kichina na serikali
za mataifa hayo mawili ya Afrika.
No comments:
Post a Comment