Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC), Joseph Kabila ameyasifu
mabadiliko yaliyoanza kuonekana katika bandari ya Dar es Salaam, na
kuihakikishia Tanzania kuwa itaongeza kasi zaidi ya matumizi ya bandari hiyo.
Kwa
mujibu wa Rais John Magufuli, hadi sasa mizigo inayopitia katika bandari hiyo
kutoka na kwenda DRC imeongezeka kwa asilimia 10.6 huku biashara baina ya nchi
hizo ikiongezeka kutoka shilingi bilioni 23 mwaka 2009 hadi bilioni 396.3 mwaka
jana.
Akizungumza na waandishi wa habari
baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais Magufuli, Ikulu Dar es Salaam jana,
Rais Kabila alisema nchi yake iko tayari kuendeleza uhusiano wa kiuchumi na
kibiashara uliopo baina ya nchi hizo mbili.
“DRC inatumia bandari ya Dar es Salaam
kwa kiasi kikubwa kusafirisha mizigo yake, lakini nikiri kuwa miaka iliyopita
tulikuwa na matatizo na bandari hii, lakini kwa kweli kwa sasa hali ni tofauti
kwani kumekuwa na mabadiliko makubwa ya huduma katika bandari hii yanayotupa
moyo,” alisema Rais Kabila.
BY: EMMY MWAIPOPO
No comments:
Post a Comment