Familia yasusia maiti mkoani geita - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, 12 October 2016

Familia yasusia maiti mkoani geita

   Image result for PICHA YA MOCHWARI
Familia  yagoma  kuchukua mwili wa marehemu  wa mzazi wao (maiti) kwa  kile kinachodaiwa wauguzi wa hospitali teule ya rufaa ya mkoa  wa Geita kuwa na majibu  machafu  kwa wagonjwa.

Akizungumza na  mtandao wa madukaonline  katika mazingira ya hospitali hiyo mmoja kati ya wanafamilia ambae  amefiwa na baba yake mzazi,Bahati Chihula  mkazi  wa  kijiji cha Kishinda kata ya Kamhanga wilayani Geita.

Amesema kuwa  walimpeleka Baba yao siku ya jumatano ya tarehe 5 mwezi huu kwa lengo la kupatiwa matibabu ya tenzi dume lakini jambo la kusikitisha  alikutana na  huduma  zisizostahili  za wauguzi   hali  ambayo imepelekea  mzazi  wake kupoteza maisha kutokana na kukosa huduma nzuri za afya.

“Tulifukuzwa katika hodi ya wagonjwa kwa madai kuwa hatutakiwi kukaa katoioka hodi hiyo na tulipotoka nje baada ya dakika chache niliporudi nilim kuta mgonjwa wangu yupo chooni na nilipouliza kwanini mgo njwa wangu yupo choo ni akiwa nagaragara mhuguzi alionijibu wewe utakiwi kujua nenda zako na kutokana na huduma mbovu za hospitari hii imepelekea kuondoa uhai wa baba yangu kwani hakuwa maututi sana na sisi kama family hatutachukua maiti paka sheria ifate mkondo wake”Alisema Bahati.

Hata hivyo moja kati ya wananchi  ambae ana mgonjwa anaye muuguza katika  hospitali  hiyo Felix  Joseph ameeleza  tatizo kubwa ni walinzi pamoja na wauguzi kwani  wamekuwa wakiwatusi wagonjwa na wananchi  wanaokuwa wakifika katika hosptali hiyo.

Kutokana na uzito wa swala hilo mbunge wa Geita vijijini  Joseph Msukuma amefikisha malalamiko hayo katika kikao cha sita cha kamati  ya ushauri  ya mkoa  kutaka  kujua utawala bora ukoje katika hospitali  hiyo na  juu  ya hatua zilizochukuliwa na mganga mkuu wa mkoa dhidi ya mgonjwa aliyefia chooni .
“Mwenyekiti nilikuwa nataka kuuliza kuhusiana na utawala bora kwenye hopstari ya Mkoa Jana mpiga kula wangu alimleta baba yake mzazi hospitarini hapo cha kusikitisha ni kwamba alifukuzwa na kutolewa nje je ni haki naomba mganga mkuu hatujibu ameshachukua maamuzi gani juu ya wale ambao wameshiriki katika kitendo hicho cha unyanyasaji”aliuliza Msukuma.

Akijibu kuhusiana na tuhuma hizo za kumwacha mgonjwa  na mwisho wa siku akapoteza uhai wake mganga mkuu wa mkoa Joseph  Kasala,amefafanua kuwa walipewa mgonjwa huyo akiwa anasumbuliwa na tenzi  dume na kwamba wakati  daktari  ambae alitakiwa  kumfanyia upasuaji  alishindwa kutokana na maumivu aliyokuwa   nayo.

Sanjari  na hayo mkuu wa mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstafu   Ezekiel  Kyunga amemwagiza mganga mkuu kwenda hospitalini hapo na kupata habari za kina na kujua  ni  nani  ambae amefanya  uzembe wa namna hiyo  na  kama mtu akibainika hatua   za  kisheria zitachukuliwa  dhidi  yake.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here