Hatua hiyo imechukuliwa siku chache baada ya kampuni hiyo ya
Korea Kusini kutangaza kwamba ingesitisha uundaji na uuzaji wa simu hizo
kutokana na kuongezeka kwa visa vya simu hizo kushika moto au kulipuka.
Mamlaka inayosimamia bidhaa na matumizi nchini Rwanda imesema
hatua ya kupiga marufuku simu hizo imechukuliwa kwa sababu za kiusalama.
"Kwa sababu za kiusalama, wateja ambao huenda walinunua
simu hizi binafsi nje ya nchi wanatakiwa kuzizima na kuzirejesha eneo
walizozinunua," imesema taarifa ya kaimu mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo
Meja Jenerali Patrick Nyirishema.

No comments:
Post a Comment