Janet Jackson na mumewe Wissam Al Mana wanadaiwa kupanga
kumpatia jina la Michael mtoto wao wa kwanza.
Wawili
hao wamepanga kumpatia mtoto wao huyo anayetarajiwa kuzaliwa mwezi ujao jina
hilo kwa madai kuwa ni kumuenzi mfalme wa muziki wa Pop duniani, marehemu
Michael Jackson pamoja na kuleta upendo kwenye familia yao.
Mpaka sasa ni miaka saba imepita
tangu kilipotokea kifo cha Michael Jackson, Juni 2009.
Taarifa za Janet kuwa na ujauzito
zilianza kusambaa mwezi Mei, mwaka huu lakini muda wote muimbaji huyo
hakuzungumza chochote mpaka pale alipoamua kufunguka kwa mara ya kwanza kwenye
tovuti ya People mwezi huu.
No comments:
Post a Comment